Home » Music » Dizasta Vina - A father figure (Official Album Intro)

Dizasta Vina - A father figure (Official Album Intro)

Written By Dizasta Vina on Thursday, Dec 28, 2023 | 08:31 AM

 
Stream/Download #AFF Intro Audiomack - https://audiomack.com/dizastavina/song/a-father-figure-official-album-intro Mdundo - https://mdundo.com/song/2790186 Other Musical contents Audiomack - https://audiomack.com/dizastavina Boom play - https://www.boomplay.com/artists/3288611 YouTube - https://youtube.com/c/dizastavina Mdundo - https://mdundo.com/a/2263 Spotify - https://open.spotify.com/artist/1IC2bcgWHOl0i4YUndZLfI Apple music - https://music.apple.com/us/artist/dizasta-vina/1572598960 Deezer - https://www.deezer.com/artist/67967532 Spotify Playlist - https://open.spotify.com/playlist/37i9dQZF1DZ06evO0XFEJi Genius - https://genius.com/DizastaVina Connect with Dizasta Vina on social medias Instagram - https://www.instagram.com/dizastavina X/Twitter - https://x.com/dizastavina Facebook - https://web.facebook.com/dizastavina07 Business: [email protected] Website - https://bio.link/dizastavina Lyrics Natazamwa kama mgongo Wa kuegewa kama chombo Nikitegemewa na watoto Lakini kwa ndani mi' ni mtoto pia Mtoto wa katikati Njiapanda kati ya Ukweli na uongo Ukubwa na udogo ama Upofu na uchongo Ama pumbazo na mwongozo Katikati ya uhalisia Na mategemeo Karibu na jitihada Mbali na egemeo Sina hesabu ya mafanikio Kila kitu ni jukumu na uwepo wangu Ndio hukumu yangu ya leo Sina cha thamani nilichorithi Ila nilichonacho ni kumbukumbu ya simulizi Na picha nilizokuwa nazo Nilizopewa na wavuja jasho Wasakatonge wa mwanzo kwahiyo Nigawie masikio yako Macho yalinipa tishio lenye manufaa kwangu Maana nilishuhudia kufanikiwa na Kushindwa kwa mashujaa wangu Lakini shuhuda zilinifunza Zilinifunza kuhusu Mashujaa Wa karibu na mbali Wenye nasibu za ghali Au watabibu wa kuponya hali Na nguvu ya kufukuza shali Za wadhalimu na waharibifu Wenye visu vikali Mashujaa walisisimua sana Lakini wapo kadhaa waliokufa Na hawakuacha alama Nilifunzwa kuhusu hawa Hawa mashujaa walipanda maua Wakilea vyema yakachipua Na wengine usingizi ulipowachukua Wadudu wala mizizi wakafukua Machache yaliyofanikiwa kukua Ndege waliyachukua Na mengine hayakuwa mahala pema Kwahiyo yalichomwa na jua na kuungua Oooh hujui walimwengu walisema nini Kuhusu hawa mashujaa wangu walioshindwa Walisema Kaharibu Kwakuwa shujaa kwa walimwengu Ni yule anayeweza wakati wa kufanya Lakini sio anayeshindwa wakati akijaribu Kwa walimwengu shujaa Ni yule mwenye nguvu Asiyetoa chozi wakati wa uchungu Asiyekosa au anayeonekana mtukufu Kwa walimwengu ushujaa ni Kuweza na sio kuthubutu Kwahiyo wakati sherehe za mashujaa Wao zikipikwa kuchochea Hadithi za mashujaa wangu Zilizikwa na kupotea Kwakuwa mashujaa wangu Hawakuvaa suti zenye nakshi na kuita Hawakuwa na viatu vya kung'ara hivyo Hawakupendeza kwenye jarida Ni kama walipima ushupavu wa mashujaa Kwa kuangalia afya za maua Bila kujua afya za maua sio ubora Wa anayeyajua pekee Lakini kuna jua na mvua na ni Ubashiri wa kujua lini vinakuja Uhakika wa kesho, kesho yenye giza Na hakuna anayeitambua Shujaa wangu alileta mlo mmoja Kuhakikisha siku haipiti, na aliweka Tofali moja wakati wa kujenga msingi Alifagia barabara alipambana na Uraibu kama kamali, ulevi na madawa Ila hadithi yake haikuvutia gazeti Sio sawa Ni vile nimeanza kuwa kama shujaa Wangu nimegundua kuwa sijamaliza kujua Ni kama nimeanza kulea wakati sikumaliza kukua Natamani kuwa shujaa mzuri Lakini nipo hapa kujifunza Na pa kuanzia sipajui Sipajui maana maelekezo ni mengi saa hii Mara jikaze wewe, baba halii Mara utapoteza nafasi, watu hawatanii Mara kwanini usifanye kama nanihii Ona mtoto wake amenanihii Bahari ya elimu ni pana kuushinda upeo Kulia matarajio, kushoto mategemeo Bado najifunza sipo mbali Ila sijui lini nitakuwa tayari Inaniwia kuweka kipimo Cha kujua kipimo kiundani Kupima usahihi na wito Ninaposema hadharani Unawaandaaje watoto kwenda mitaani Kwa sababu kuliko kuwa mkata maua vitani Ni bora kuwa mwanajeshi kwenye bustani Nini maana ya kuwa baba Ikiwa bado najifunza Kutosherehekewa nikishinda Ila kusakamwa nikianguka? Hata nikipendwa au nikichukiwa Ni sawa ila si vyema nikapuuzwa nimechelewa ila ni vyema Nimejua kuwa baba hazaliwi Anaundwa