Home » News & Politics » Waziri Mkuu katoa saa 72, kwa Mkurugenzi na Mweka Hazina wa Halmashauri ya Ukerewe.

Waziri Mkuu katoa saa 72, kwa Mkurugenzi na Mweka Hazina wa Halmashauri ya Ukerewe.

Written By Millard Ayo on Sunday, Feb 18, 2018 | 12:47 PM

 
Leo kwa mara ya kwanza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea Wilaya ya Ukerewe na kabla ya kuanza ziara yake akaongea na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ambapo Waziri Mkuu ametoa saa 72 kwa Mkurungezi wa Ukerewe Frank Bahati pamoja na mweka hazina wa Halmashauri Peter Kishau kutoa majibu ya Pesa jumla ya mil. 257.5, hazijulikani zilipo. Serikali ilitoa Pesa za miradi mil.425, Pesa mil.221.5 hazijulikani zilipo, madai ya Walimu mil.84, mil.23 hazijulikani zilipo pamoja na Pesa za Watumishi mil.56 ,Pesa mil.13 hazijulikani zilipo.