Home » News & Politics » KAMPENI TFF: Sera za Iman Madega akipewa Urais wa TFF

KAMPENI TFF: Sera za Iman Madega akipewa Urais wa TFF

Written By Millard Ayo on Wednesday, Aug 09, 2017 | 01:55 PM

 
Mwenyekiti wa zamani wa chama cha soka mkoa wa Pwani na club ya Dar es Salaam Young Africans mwanasheria Iman Madega ni miongoni mwa wagombea Urais wa TFF waliyozindua kampeni zao za kuomba kura za Urais leo kupitia vyombo vya habari. Iman Madega ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea na anakampuni yake, ameomba kura na kunadi sera zake akidai kuwa wakimpa nafasi ya kuwa Rais wa TFF atachukua likizo ya kazi yake ya uanasheria ili kulitumikia soka pekee maana mpira wa miguu kwa sasa unahitaji muda zaidi.