Download and stream The lost one
Spotify - https://open.spotify.com/track/4tIhbGMorjRbeGLYaUUJZo
Mdundo - http://mdundo.com/song/83278
Apple music - https://music.apple.com/us/album/the-lost-one/1574590028?i=1574590029
Boomplay - https://www.boomplay.com/songs/64659519?srModel=COPYLINK&srList=WEB
Dizasta vina on social networks
https://www.facebook.com/dizastavina07
https://www.instagram.com/dizastavina
https://www.twitter.com/dizastavina
Follow PanoramaAuthentik on social networks
https://www.twitter.com/panauthentik
https://www.instagram.com/panoramaauthentik/
https://www.facebook.com/PanoramaAuthentik/
Music video by Dizasta Vina performing The lost one
(C) 2019 PanoramaAuthentik™
Lyrics
Alivaa sketi inayoangaza ilikuwa nyepesi
Fupi unaweza dhani ni kidenti
Japo nilikuwa single ila sikuwa mingle alizidisha maringo alipogundua namcheki
Haiba ya aibu mfumo wa kibinti
Kidogo rangi na lile umbo la kimisi
Akiweka pozi nihakiki
Alikuwa anang'aa ila ngozi yake ilisanifu dhiki
Bado ilikuwa hainiboi kumtazama
Macho yangu yalikuwa yana-enjoy alichofanya
Kiasili nilikuwa hoi (hoi) kiasi cha kutogundua alikuwa na konvoi la mimama
Kwa mtindo wa kujongea kwa madaha
Yule malaika akaanza kusogea nilipokaa
Hata kabla sijaamua kumchunguza
Macho yaligundua kuwa binti anajiuza
Hiyo iliweka ufa moyoni
Nilitamani hata kustuka ndotoni
Kwakuwa nilipata hisia kali za upendo
Nikawa tayari hata kujitupa motoni
Nilitekwa i only needed her for the rescue
That's how far love can take you
Nikataka mpaka kumvika pete
Awe mchumba nikasahau mwenzangu anawaza cash tu
Ni aina ya wasichana wanaotokea kwenye ndoto
Yaani unafumba macho alafu unaona anakulelea watoto
Kwa mara ya kwanza maishani mwangu niliwaza ndoa, Hasa baada ya mapenzi ya wasichana wa town kuniboa
Akiongozana na kundi la wenzake
Akasogea akitoa sauti za kipambe
Kila mmoja akijinadi kwa mikogo ya mahaba
Nakumbuka mmoja alivua brauzi nimtomase
Alijinadi kama ng'ombe mnadani
Nikataka nijitose chakani,
Yaani nijitoe sadaka nilimwona
Ka' kidani cha dhahabu maisha ya mjini yalifanya ajione hana thamani
Tukagonganisha macho kihisia
Ndio nikajua nimezama na sijui nitakapoishia
Apendae kipofu nikazisahau kasoro
Nikashuka nikamfungulia mlango akaingia
Kwa pupa nikadrive mpaka home
Nilipofika hata kuzima gari sikukumbuka
Kuna muda nilimkuta uchi kitandani
Anauliza ka' tunaenda kavu au kwa ndom. Huh
Nikamsihi avae nguo
Akahamaki akauliza maswali mawili kwa mkupuo
Jogoo hawiki braza au ume-mix machaguo
Nikamjibu mi msafiri na we' binti ndo' kituo
Kwa jicho la kufuga kisasi
Akanicheki kiasi kwamba niliyumba kinafsi
Akanikumbusha hajaja kwangu kutafuta hifadhi
Anafanya biashara na kwangu amekuja kikaz
Nikashika usemi uchafu ukiingia kwenye kapu toa
Usitupe kapu kwahiyo sikumwona kama changudoa
Nikamwambia nikimwangalia kwanza nawaza kujenga pili familia na tatu ndoa
Hakuitikia akanitenga na himaya ya majibu,
Moyo wake haufunguki na ninahitaji rai
Hatukuwa sawa nilitaka kujaribu, akanijibu Kipepeo na nyuki hawatagi yai
Akaniruhusu kumkumbatia,
Akashika mikono yangu akaibusu kwa hisia
Sijui alinipa nini nilijikuta naanguka
Kizunguzungu ile kustuka kumekucha
Niliamka na mawenge kichwani
Nilighafirika kugundua hakwepo chumbani
Aliondoka aliniacha na aibu mtaani
Maana aliposepa alibeba kila kitu ndani.
Alikuwa kunguru na nilisahau hafugiki
Hata iwe kibudu kwa nyanya na limao haungiki
Alibeba vipi sijui kinachoniuma
Ni kukosa pendo la huyu binti.
Sitasahau macho yake mawili ya kirembo
Sauti iliyowasilisha upendo
Akipigwa vikali na ubatili wa matendo ya mwili wake mzuri ambao haustahili mateso
Aliniachia meseji alipoondoka,
Akinipa pongezi kwamba sikuwa mwoga, kuufuata moyo wangu akaniomba msamaha akisema hawezi kuenzi penzi ambalo kwa wazazi alikosa
Sawa ah! Nimekusamehe zamani mami,
Pendo lako dawa ewe baniani,
Niahidi utawasamehe wazazi wako pia
Ambao wamefanya uonekane shetani honey. Yeah
I'm kinda lost I do things i ain't suppose to
I thought you'll be my best friend that I can talk to,
I wanna change if you wanna change I'll support you
I think we both need the way out that we can walk through.
Ah popote ulipo ambapo info inafika,
Bado mrume nipo miaka inapita nauandika huu wimbo umenifundisha nisitue mzigo kama ninahisi sijafika.
Naoa kesho na nina hamu kukukuta
Nikwambie dunia safi binadamu ndo' uchafuka,
Ni kawaida usisahau kutabasamu kukikucha,
Nakuombea afya kwenye nyama damu na mifupa