“NI MARA NGAPI UNATAKIWA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WIKI!”
Kabla hatujaainisha namba halisi ni mara ngapi unashauriwa kufanya sex unapaswa kufahamu mambo yafuatayo.
Kila mtu ameumbwa tofauti: Vivyo hivyo na mahitaji ya sex pia huwa tofauti kwa kila mtu. Umri, Uimara wa mwili, afya ya mwili na kiwango cha hisia hutofautiana kati ya mtu na mtu. Kitu cha muhimu zaidi kwa wenza ni kuwepo kwa mawasiliano ya wazi juu ya hitaji muhimu la kila mmoja wenu ili kupanga na kuamua muda na vipindi sahihi vya kufurahia sex.
Ubora wa sex ni muhimu zaidi kuliko idadi ya kusex: Msiwekeze akili yenu kwamba ni lazima muende round kadhaa, bali wekezeni akili yenu ni kwa namna gani mnaweza kufurahia sex wote wawili bila kujali mmeenda round ngapi. Na hili linaweza kufanikiwa ikiwa kuna mazungumzo ya wazi baina ya wapenzi. Msifanye sex kwa lengo la kuoneshana umwamba bali fanyeni kwa kufurahi.
Msiwekeane matarajio makubwa kila siku: Miili yetu hupitia vipindi tofauti, kuna wakati hamu ya kusex huwa ni kubwa kuliko vipindi vingine. jifunzeni kuving’amua vipindi hivyo na mambo ambayo husababisha vipindi hivyo kutokea ili kama kuna uhitaji wa kusaidiana, basi msaidiane na muendelee kufurahia sex.
Kubali mabadiliko na uwe mbunifu: Hisia ya kusex hubadilika mara kwa mara, sio kila siku mwenza wako atakuwa na hamu na wewe. Hata hivyo ubunifu, uaminifu, kujaribu vitu vipya na heshima vinaweza kuongeza hamu na hisia baina ya wapenzi.
Sex inahusisha hisia zaidi: Sex sio kwa ajili ya kuufurahisha mwili pekee! Bali ni jambo linalohusisha kuziteka hisia za mwenza wako. Fanya mambo ambayo yatatengeneza muunganiko mzuri kati yako na mwenza wako, michezo ya hapa na pale, kupigana mabusu, utani, kukumbatiana na stori za kimahaba ni baadhi ya mambo yanayoweza kuongeza hamu ya kila mmoja wenu.
Ikiwa umependezwa na somo hili basi usiache kulike, kushare na kusubscribe kwenye channel yetu kwa masomo zaidi.
Kwa maoni au maswali tumia uwanja wa koment na tutakufikia mara moja.