Home » Entertainment » Bei Ya Chakula Kushuka: Wizara Ya Kilimo Yaahidi Kupunguza Bei Ya Unga Na Mchele Februari

Bei Ya Chakula Kushuka: Wizara Ya Kilimo Yaahidi Kupunguza Bei Ya Unga Na Mchele Februari

Written By Ebru TV Kenya on Tuesday, Jan 03, 2023 | 11:00 AM

 
Waziri Wa Kilimo Mithika Linturi Hii Leo Ametoa Hakikisho Ya Kwamba Kufikia Mwezi Wa Pili Mwaka Huu Bei Ya Vyakula Kama Vile Mchele Na Unga Wa Ugali Itashuka. Waziri Alitaja Hili Litawezakana Kupitia Mpango Ambao Serikali Ya Kenya Kwanza Imeweka Kusaidia Wakulima Kuimarisha Uzalishaji Wa Chakula Nchini, Pamoja Na Uagizaji Wa Vyakula Kama Vile Mahindi Na Maharagwe Kutoka Mataifa Ya Nje Ili Kupunguza Makali Ya Njaa Iliyosababishwa Na Ukame. Waziri Linturi Pia Amejitenga Na Semi Za Waziri Wa Viwanda Na Biashara Ya Novemba Mwaka Jana Kuhusu Uagizaji Wa Vyakula Vya GMO Nchini.