Home » Education » Ufanisi wa barakoa mbali-mbali katika kuzuia maambukizi ya korona - uchambuzi wa utafiti

Ufanisi wa barakoa mbali-mbali katika kuzuia maambukizi ya korona - uchambuzi wa utafiti

Written By Dr Mwidimi Ndosi on Wednesday, Dec 28, 2022 | 11:18 AM

 
Tumefanya uchambuzi wa utafiti kuhusu ufanisi wa barakoa mbali-mbali katika kuzuia maambukizi ya korona. 0:00 - Mwanzo 0:20 - Jumbe kuu mbili 1:18 - Lengo la utafiti 1:36 - Aina ya utafiti 2:46 - Washiriki 4:41 - Kukusanya data 5:25 - Mchakato wa data 9:44 - Wasifu wa washiriki 10:29 - Matokeo ya utafiti 15:07 - Hitimisho na ujumbe mkuu Utangulizi Kuvaa barakoa na hasa zile zenye ubora wa hali ya juu inashauriwa maana imeonekana katika tafiti za maabara, kwamba hizi barakoa zina uwezo mkubwa wa kuzuia virusi kupenyeza. Kwa kuwa mazingira ya maabara hayafanani na maisha ya uhalisia ni muhimu kufanya utafiti katika jamii ili kuhakikisha kwamba matokeo ya utafiti yatasaidia katika uhalisia wa maisha ya kawaida. Huu utafiti wa Andrejko na wenzake (2022) uliangalia ufanisi wa barakoa katika kuzuia maambukizi ya virusi vya korona katika kumbi zenye mijumuiko ya watu. Matokeo ya utafiti 1. Utumiaji wa barakoa kwenye mikusanyiko ya watu katika mazingira ya ndani ulihusiana na uwezekano mdogo wa kupata maambukizi kuliko kutovaa barakoa kabisa. Uwezekano wa kupata maambukizi baada ya kuweka uwiano (adjustments) kati ya makundi haya mawili [aOR] = 0.44; 95% CI = 0.24–0.82). Hii yaonyesha kuwa uwezekano wa kupata maambukizi endapo kama barakoa ya aina yoyote imetumika unapungua kwaa asilimia 56 (au -56%), ukilinganisha na kama barakoa haikuvaliwa kabisa. 2. Katika washiriki 534 walioainisha aina ya barakoa walizotumia, ukilinganisha na kutovaa barakoa kabisa, uvaaji wa barakoa za hali ya juu (N95/KN95) na barakoa za upasuaji (surgical masks) vilihusiana na kupungua uwezekano wa maambukizi. Uwezekano wa kupata maambukizi baada ya kuweka uwiano kati ya makundi mawili Barakoa za hali ya juu (N95) vs kutovaa kabisa (aOR = 0.17; 95% CI = 0.05–0.64) - uwezekano wa kupata maambukizi endapo kama barakoa ya hali ya juu imetumika unapungua kwa asilimia 83% (au -83%), ukilinganisha na kama barakoa haikuvaliwa kabisa. Barakoa za upasuaji vs kutovaa kabisa barakoa (aOR = 0.34; 95% CI = 0.13–0.90) - uwezekano wa kupata maambukizi endapo kama barakoa ya upasuaji imetumika unapungua kwa asilimia 66% (au -66%) , ukilinganisha na kama barakoa haikuvaliwa kabisa. 3. Ukilinganisha na kutovaa barakoa kabisa, uvaaji wa barakoa za kitambaa ulizuia kidogo tu uwezekano wa maambukizi. Uwezekano wa kupata maambukizi baada ya kuweka uwiano kati ya makundi mawili Barakoa za kitambaa vs kutovaa barakoa kabisa (aOR = 0.44; 95% CI = 0.17–1.17) - uwezekano wa kupata maambukizi endapo kama barakoa ya kitambaa imetumika unapungua kwa asilimia 56% (au 56%), ukilinganisha na kama barakoa haikuvaliwa kabisa. Lakini huu uwezekano haujafikia kiwango cha kutambulika kama cha umuhimu wa kitakwimu (achieving statistical significancy) Ujumbe mkuu 1. Matokeo haya yanaonesha kwamba pamoja na kupata chanjo za UVIKO-19, uvaaji wa barakoa mara zote na wakati wote mtu akiwa sehemu za ndani zenye mkusanyiko wa watu hupunguza uwezekano wa kueneza maambukizi ya korona 2. Uvaaji wa barakoa za hali ya juu (N95) humpa mvaaji kinga ya hali ya juu zaidi ya kuvaa barakoa za kitambaa au kutovaa kabisa. Andrejko KL, Pry JM, Myers JF, et al. Effectiveness of Face Mask or Respirator Use in Indoor Public Settings for Prevention of SARS-CoV-2 Infection — California, February–December 2021. Morbidity and Mortality Weekly Report. 2022;71(6):212-216. https://dx.doi.org/10.15585/mmwr.mm7106e1