Home » News & Politics » Mjane wa marehemu ajali ya moto wa mafuta Morogoro asimulia ugumu wa maisha

Mjane wa marehemu ajali ya moto wa mafuta Morogoro asimulia ugumu wa maisha

Written By Azam TV on Sunday, Aug 28, 2022 | 06:14 AM

 
Zisikie panda shuka, chungu tamu anazokutana nazo Ashura Ramadhan mkazi wa mtaa wa Sina Mkoani Morogoro. Ashura ni mjane wa mume ambaye alifariki kwenye ajali ya moto uliosababishwa na lori la mafuta eneo la Msamvu mkoani Morogoro Agosti 10, 2019 na kupoteza maisha ya zaidi ya watu 90. Mjane huyo anatusimulia namna ambavyo ajali hiyo imesababisha maisha yake na wanawe kuwa magumu hadi sasa.