Home » People & Blogs » WANANCHI KATA YA IGIMA , KUNUFAIKA NA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

WANANCHI KATA YA IGIMA , KUNUFAIKA NA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

Written By MLIMBA TV on Friday, Nov 05, 2021 | 12:39 PM

 
Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 500= kwa ajiri ya ujenzi wa kituo cha Afya katika kata ya igima katika halmashauri yawilaya mlimba mkoani morogoro . Haya yamezungumzwa leo tarehe na afisa mtendaji wa kata ya igima , Edna LILEWA akiwa na kamati ya maendeleo ya kata hiyo baada ya kukagua eneo la hekari nane na nusu kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya cha kata kitachojengwa katika kitongoji cha malumbo. Bi lilewa amesema kuwa kufuatia ujenzi wa kituo hicho cha afya kata igima inatarajiwa kuanza hivi karibuni na tayari serikali imetoa shilingi milion 330 ili kuanza kwa ujenzi huo,nakuongeza kuwa wamekubaliana na baadhi ya wananchi kuachia maeneo yao ya mashamba kwa kulipwa fidia ili kutumika kwa ujenzi huo , jambo ambalo litaondoa adha kwa wananchi wa kata hiyo kwakukosa huduma ya afya kwa ukaribu .