Home » People & Blogs » KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA FRIDAY PRAYERS 26/02/2021

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA FRIDAY PRAYERS 26/02/2021

Written By Rev. Dr. Eliona Kimaro on Friday, Feb 26, 2021 | 01:54 PM

 
KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA FRIDAY PRAYERS 26/02/2021 UJUMBE WA LEO: "NJIA YAKO DUNIANI" "YOUR WAY UPON THE EARTH" "NAMI NAWAREHEMU MAELFU ELFU" Mwanzo 20 : 17 - 18 Kutoka 20 : 5 - 6 Yoeli 2 : 12 - 14 Luka 23 : 42 - 43 Mwanzo 20 : 17 - 18 17 Ibrahimu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana. 18 Maana Bwana alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu. Kutoka 20 : 5 - 6 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. Yoeli 2 : 12 - 14 12 Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; 13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya. 14 N'nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu? Luka 23 : 42 - 43 42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. 43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi. Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: [email protected]