Home » News & Politics » AFISA ELIMU DAR 'AWAPA MAKAVU' WALIMU VIBURI

AFISA ELIMU DAR 'AWAPA MAKAVU' WALIMU VIBURI

Written By MwanaHALISI TV on Monday, Oct 05, 2020 | 08:13 AM

 
Wakuu wa Shule za Sekondari Kanda ya Dar es Salaam wametakiwa kuitumia Makumbusho ya Taifa nchi kama nyenzo muhimu ya kufundishia ili kuongeza uwelewa wa haraka kwa wanafunzi kama njia moja wapo itakayo saidia kufikia malengo ya kuondoa ziro nchini. Hayo yamesemwa na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Abdul Maulid alipokuwa akifungua Mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari Kanda ya Dar es Salaam. Amesema kuwa Rais John Pombe Magufuli anawapenda walimu hivyo, wanatakiwa wafanye kazi kwa bidii ili kutokomeza ziro. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga ameeleza namna ambavyo Taasisi hiyo inavyoinufaisha sekta ya elimu nchini. 🔘JE, NA WEWE UNA HABARI? 🔘WASILIANA NA MwanaHALISI TV ( +255 767 400402), 🔘WhatsApp ( +255 692 318213) 🔘Email: [email protected] 🔘KWA HABARI ZA KILA SIKU: http://mwanahalisionline.com