Home » News & Politics » MSIBA MZITO DAR || MUME ADAIWA KUMUUA MKE WAKE KWA KIPIGO

MSIBA MZITO DAR || MUME ADAIWA KUMUUA MKE WAKE KWA KIPIGO

Written By Mwananchi Digital on Monday, Aug 24, 2020 | 02:09 PM

 
“Walikuwa ni watu wenye upendo, huwezi kudhani kama kuna ugomvi ndani yao na hata tuliposikia taarifa hizi zilitushtua,” Ndivyo alivyoanza kusema mmoja wa majirani wa marehemu Agnes Mushi ambaye alipoteza maisha usiku wa kuamkia jumamosi ya Agosti 22, 2020 kwa kile kilichosadikika kuwa aliuliwa na mume wake Jeremiah Duma. Agnes (35) ambaye ni mama wa watoto watatu alikuwa mjasiriamali, mwenye ukaribu na majirani na mwepesi wa natatizo ya watu. Akizungumza na Mwananchi Kamanda wa Polisi Kinondoni, Edward Bukombe alisema ni tukio hilo limetokea na chanzo kikubwa ni ulevi na wivu wa mapenzi.