Home » Howto & Style » Purity Wanjiru: 'Nilikuwa kahaba nikiwa kwenye ndoa'

Purity Wanjiru: 'Nilikuwa kahaba nikiwa kwenye ndoa'

Written By BBC News Swahili on Wednesday, Jul 08, 2020 | 06:51 AM

 
Purity Wanjiru ni mwanamke aliyezaliwa katika familia ya watoto 12 akiwa kitinda mimba nchini Kenya. Wanjiru hakupenda kwenda shuleni na siku moja familia yake yote iliamua kumuadhibu kwa viboko na kutokana na hilo aliamua kutoroka kwao nyumbani akiwa na miaka 13 na kuamua kuishi mitaani. Baada ya muda alipata mwanamume anayedai kuwa hakuwa anawajibika kwa namna yoyote ile. Marafiki zake walimshauri njia ya kupata pesa ni kushiriki ukahaba na kulingana na Purity ni kazi aliyoifanya hadi alipopata kifungua mimba wake. Mume wake alifahamu kazi aliyoifanya ya ukahaba kwani pesa hizo ndizo walikuwa wakitumia kuyakidhi maisha yao wote watatu. #Wanawake #bbcswahili #waridiwabbc