Home » Entertainment » MATESO YA YESU SEHEMU YA TANO: IJUMAA KUU - NJIA YA MSALABA MPAKA KIFO CHA YESU

MATESO YA YESU SEHEMU YA TANO: IJUMAA KUU - NJIA YA MSALABA MPAKA KIFO CHA YESU

Written By Jugo Media Network on Friday, Apr 10, 2020 | 12:00 AM

 
Msalaba wa Yesu Jump to navigationJump to search Mchoro wa Diego Velázquez, Yesu msulubiwa, 1631, Prado (Madrid, Hispania) unaonyesha anwani juu ya kichwa chake. Kigae cha msalaba - Basilica di Santa Sabina huko Roma (Italia). Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu Jesus [ficha]Yesu Kristo na Ukristo Umwilisho • Utoto wa Yesu • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu • Miujiza ya Yesu Msalaba wa Yesu • Kifo cha Yesu • Ufufuko wa Yesu Kupaa mbinguni • Ujio wa pili Injili • Majina ya Yesu katika Agano Jipya • Yesu kadiri ya historia • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia [ficha]Mazingira ya Yesu Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Yohane Mbatizaji [ficha]Mitazamo juu ya Yesu Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa This box: onyeshamajadilianohariri Msalaba wa Yesu ni msalaba ule ambao Yesu Kristo alisulubiwa juu yake huko Yerusalemu kwa amri ya Ponsyo Pilato siku ya Ijumaa, labda tarehe 7 Aprili 30 BK. Tukio hilo, pamoja na ufufuko wa Yesu unaosadikiwa na Ukristo kutokea siku ya tatu (Jumapili ya Pasaka), ndiyo kiini cha imani ya dini hiyo mpya iliyotokana na ile ya Uyahudi. Kwa Wakristo fumbo hilo la Pasaka ndilo kilele cha historia ya wokovu inayotangazwa na Biblia ya Kikristo. Fumbo hilo lilisababisha kazi nyingi za sanaa ya Kikristo, hasa uchoraji na uchongaji. Historia Adhabu hiyo kali ilianza kutumika huko Uajemi na kuenea hadi Dola la Roma ambalo liliitumia hasa katika maeneo ya pembeni na kwa watumwa. Kadiri ya Injili zote nne, Ponsio Pilato, liwali wa Palestina (26-36), aliamua Yesu aadhibiwe hivyo kulingana na shtaka la viongozi wa Wayahudi waliodai kwamba mtuhumiwa alijitangaza kuwa mfalme na kupinga mamlaka ya Kaisari wa Roma, kwa wakati huo Tiberius, ingawa Pilato alikuwa ametambua shtaka halikuwa la kweli, bali lilitokana na husuda. Kadiri ya Injili ya Yohane, Pilato mwenyewe alisisitiza kwamba, katika maandishi yaliyotakiwa kuwajulisha watu sababu ya adhabu hiyo, iwekwe wazi kwamba Yesu aliuawa kama mfalme wa Wayahudi, ingawa neno hilo lilichukiza viongozi wa taifa.