Home » News & Politics » SHUHUDIA MAFURIKO YALIVYONG'OA RELI "TUMESITISHA HUDUMA RELI YA KATI"

SHUHUDIA MAFURIKO YALIVYONG'OA RELI "TUMESITISHA HUDUMA RELI YA KATI"

Written By Millard Ayo on Wednesday, Feb 05, 2020 | 08:12 AM

 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesitisha huduma za usafiri wa treni ya abiria na mizigo kutokana na uharibifu wa njia za reli uliosababishwa na mafuriko maeneo ya Kilosa, Igandu, Dodoma na Makutupora. "Kutokana na hali hiyo hiyo ya uharibifu wahandisi wa TRC wako katika maeneo mbalimbali yaliyoharibika kufanya tathmini halisi ya gharama za miundombinu ya reli iliyoathirika, matengenezo ya muda mfupi yanaendelea," amesema Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa Amesema kuwa maeneo yaliyopata uharibifu mkubwa ni Kilosa, Gulwe(Mpwapwa), Igandu, Zuzu na Makutupora.