#KonaYaKiufundi Simba dhidi ya Biashara utd
.
1. Mechi ilikuwa nzuri na ya wazi,huku ikitawaliwa na mbinu zaidi,lakini kila aliyeutazama mchezo huu hakika atakuwa amefurahia burudani
.
2. Simba kama ilivyo kawaida yao walikuja na 4:4:2 diamond ambayo imeonekana kukubali kwa siku za karibuni,plani yao kubwa ni kucheza kwenye eneo ambalo mpinzani wake anapaswa kutulia na kufanya ubunifu,kasi waliyoanza nayo leo ilikuwa ya kawaida sana ukilinganisha na mchezo uliopita na hiyo ni kutokana na ubora waliokuwa nao Biashara utd,uwepo wa Bocco na Kagere unaendelea kuwa tatizo kwa timu pinzani na kutoa uhuru kwa viungo washambulizi wake kwa maana ya Chama,Kahata na Mikisson,lakini pia fullback wa simba wanaongeza option kwa viungo hao kutokana na kasi na ubora wao...
.
3.Biashara walikuja na gemu plani nzuri,walijua simba wanatengeneza mashambulizi yao kuanzia chini,basi na wao wawe wengi zaidi kwenye eneo la juu,kipindi cha kwanza ni kama walifanikiwa kutokana nidhamu waliyokuwa nayo kwenye kufanya marking wanapokuwa out of possesion,closing down yao ni kama ilikuwa double standard,tuicompact timu lakini utaona kuna maeneo ambayo walijua wakiupata mpira wanaupeleka,zile counter boxing zao zilikuwa za hali ya juu utaona ndani ya dakika 30 walikuwa na ontarget 3
.
4. Luis Mikisson 🙌🙌 anaendelea kuonyesha thamani yake akiwa na jezi ya Simba,anafanya movement za hatari sana,mpira unatii anachokitaka,bado hakuna strategy ya timu kumzunguka huyu mtu,Simba kama wataamua kucheza kwa kumzunguka huyu mtu basi itakuwa ni balaa..
.
5. Kwenye eneo la kati la Biashara kuna mjasiriamali anaitwa Novatus Dismas 🙌🙌 anavaa jezi namba 40,ni bwana mdogo sana lakini ana shuhuli kwelikweli,utaona leo movement nyingi za Chama zilikuwa salama sana kwa Biashara,bwana mdogo aliweza kufanya kile ambacho viungo wengi wakicheza dhidi ya Chama hawawezi kukifanya...
.
6. Atupele ni kweli kuna kitu ameongeza kwenye mstari wa washambuliaji wa Biashara,alifanya kazi nzuri sana leo..Golikipa wa biashara 🙌🙌ni mtu na nusu,positioning,goalkeeping yake ni ya hali ya juu..
.
NB: Mmakonde wa Simba amejua kutulaza mapema..🤔
.
#bakinasisi__ #njookwetu #TupoNawePaleUlipo