Home » News & Politics » Kata ya Mikocheni yafanya ukaguzi wa leseni za biashara.

Kata ya Mikocheni yafanya ukaguzi wa leseni za biashara.

Written By EastAfricaTV on Tuesday, Apr 30, 2019 | 10:42 AM

 
Afisa mtendaji wa kata ya Mikocheni jijini Dar es salaam Bw. Salum Mzaganya akiwa na maafisa wengine wa serikali za mitaa katika kata hiyo leo wamefanya zoezi la ukaguzi wa leseni za biashara kwa maduka yaliyopo ndani ya kata ya Mikocheni kwa lengo la kuwabaini wakwepa kodi. Akizungumza na Kurasa katika zoezi hilo la ukaguzi Mzaganya amesema ofisi yake imebaini pia kuwepo kwa baadhi ya nyumba za kuishi watu ambazo zimepangishwa kama ofisi kwa lengo la kukwepa kulipa kodi za serikali.