Home » Sports » Kagere alipowatungua Yanga kuwapa Simba pointi tatu

Kagere alipowatungua Yanga kuwapa Simba pointi tatu

Written By Azam TV on Saturday, Feb 16, 2019 | 01:10 PM

 
Simba SC ilipowatetemesha watani wao wa jadi Yanga SC kwa kipigo cha bao 0-1 katika mchezo mkali uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Bao pekee la Simba limefungwa na Meddie Kagere dakika ya 71 kwa kichwa akimalizia krosi ya John Bocco na kuamsha shangwe za kutosha kwa mashabiki wa timu hiyo waliofurika ndani ya Dimba la Taifa. Mara baada ya mchezo, kiungo wa Yanga, Feisal Salum, amesema Simba wamekuwa na bahati kwa kutumia nafasi waliyoipata na wao hawakati tamaa kwenye mbio zao za ubingwa wa ligi kuu msimu huu. Kwa upande wake mfungaji wa bao pekee la Simba Meddie Kagere amesema tayari wameshayasahu matokeo hayo na sasa wanajipanga kwaajili ya mchezo ulio mbele yao huku akiwajibu wanaobeza umri wake akisema kuwa akili ya uwanjani ni muhimu kuliko umri. Baada ya matokeo hayo Simba imefikisha pointi 39, ikiwa ni pointi 19 nyuma ya vinara Yanga huku Azam wakiwa nafasi ya pili na pointi 49.