Home » News & Politics » "Haitakuwa na mibonyeo" - Mfugale amwaga sifa za barabara ya njia nane Kimara-Kibaha

"Haitakuwa na mibonyeo" - Mfugale amwaga sifa za barabara ya njia nane Kimara-Kibaha

Written By Azam TV on Thursday, Dec 20, 2018 | 06:27 AM

 
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Desemba, 2018 ameweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro Jijini Dar es Salaam katika sehemu ya kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye urefu wa Kilometa 19.2. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale pamoja na kubanisha sifa za kitaalamu za barabara hiyo, amesema upanuzi huo utasaidia kupunguza msongamano mkubwa wa magari takribani 50,000 yanayopita katika barabara hiyo kwa siku na utaokoa muda kutoka saa tatu zinazotumika kupita eneo hilo kwa sasa hadi nusu saa. Amebainisha kuwa upanuzi wa barabara hiyo utafanyika kwa muda wa miezi 30 kuanzia tarehe 21 Julai 2018 na utagharimu shilingi Bilioni 141.56, fedha zote zinatolewa na Serikali ya Tanzania.