Home » News & Politics » GLOBAL HABARI OCT 08: IGP ashusha rungu kwa askari waliosindikiza kahawa ya magendo

GLOBAL HABARI OCT 08: IGP ashusha rungu kwa askari waliosindikiza kahawa ya magendo

Written By Global TV Online on Monday, Oct 08, 2018 | 12:31 PM

 
#GLOBALHABARI GLOBAL HABARI OCT 08: IGP ashusha rungu kwa askari waliosindikiza kahawa ya magendo MKUU wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Siro amemtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Augustino Olomi kuwachukulia hatua askari wote wa Polisi wa wilaya ya Kyerwa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo Justine Joseph kwa tuhuma za kusindikiza kahawa ya magendo kwenda nchi jirani. Msemaji wa jeshi la polisi Barnabas Mwakalukwa amesema kuwa IGP Siro ametuma kikosi maalumu kutoka makao makuu ya Polisi Dar es Salaam ili kwenda kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo. Pia IGP Siro amefanya maamuzi ya kumuamisha mkuu wa polisi wa wilaya hiyo na kwenda kufanya kazi katika kituo kingine ili kupisha uchunguzi huo. IGP Siro amewataka askari wengine wa Polisi nchini kufanya kazi kwa weledi bila kuvunja sheria kanuni na taratibu za jeshi hilo pamoja na sheria za nchi. Katika hatua nyingine Mwakalukwa amelitolea ufafanuzi suala la upotevu wa Mtoto wa Mhariri wa Gazeti la Uwazi Elvan Stambuli, Christopher Stambuli. GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOKInstall