Home » News & Politics » Waziri Mkuu atoa siku 30 kulivunja Baraza la Madiwani Kigoma Ujiji, aeleza sababu

Waziri Mkuu atoa siku 30 kulivunja Baraza la Madiwani Kigoma Ujiji, aeleza sababu

Written By Azam TV on Sunday, Jul 29, 2018 | 11:02 AM

 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku 30 kwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kujirekebisha na kumaliza tofauti zao ndani ya siku 30 na iwapo wataendelea na vurugu Serikali haitosita kuvunja baraza la Madiwani. Amesema hatua hiyo inatokana na Madiwani hao kutumia muda mwingi wakigombana badala ya kuwahudumia wananchi, Serikali inataka kuona wananchi wakihudumiwa kwa kuboreshewa maendeleo katika maeneo yao na si kushuhudia viongozi wakigombana kwa maslahi binafsi. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo (Jumamosi, Julai 28, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kigoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenye uwanja wa Kawawa, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kigoma.