Home » Entertainment » Waziri Kigwangalla atoa siku 90 wahusika kufanya sensa ya Mamba

Waziri Kigwangalla atoa siku 90 wahusika kufanya sensa ya Mamba

Written By Millard Ayo on Monday, Jul 02, 2018 | 10:51 AM

 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamisi Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kufanya utafiti na sensa ya mamba katika ziwa Rukwa ili kubaini idadi yake na hatimaye kuishauri Serikali namna ya kudhibiti madhara yanayosababishwa na mamba hao kwa wananchi hususani katika jimbo la Songwe na ikibidi kuwavuna kama idadi yao itabainika kuwa kubwa.