Home » News & Politics » Mbowe, Lema Walivyotinga Mahakamani Leo

Mbowe, Lema Walivyotinga Mahakamani Leo

Written By Global TV Online on Tuesday, May 15, 2018 | 07:41 AM

 
Mbowe, Lema Walivyotinga Mahakamani Leo MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeanza kusikiliza kesi dhidi ya Mbowe na viongozi wenzake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambapo wanakabiliwa na mashitaka ya kufanya mikusanyiko isiyo halali. Mahakama hiyo imeyatupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake nane ya kutaka kesi yao ipelekwe Mahakama Kuu kwa sababu hayana mashiko. Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na kuipanga kesi hiyo kesho Mei 16,2018 saa nane mchana kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali (PH). Wakati uamuzi huo ukisomwa na Hakimu Mashauri mahakamani walikuwapo washtakiwa, Freeman Mbowe, mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika. Mbunge wa Tarime mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche. Kwa upande wa Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Ester Bulaya hawakuwepo mahakamani ambapo Wakili Peter Kibatala alieleza kuwa walikuwa safarini kutoka Dodoma kuja Dar es Salaam kuhudhuria kesi lakini wakaharibikiwa na gari. Pia Wakili Kibatala aliiomba mahakama kuipanga kesi hiyo kwa ajili ya washtakiwa kusomewa PH Juni 8 ama 15, 2018 kwa sababu wao mawakili watakuwa katika kesi Mahakama Kuu. Baada ya Kibatala, kuwasilisha hoja hiyo Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiomba wawasomee maelezo ya awali washtakiwa hao kesho Mei 16,2018 . Nchimbi alidai kuwa hoja iliyowasilishwa na wakili Kibatala kuwa wana kesi Mahakama Kuu imekuja kwa maneno matupu na kwamba angalia wangeiwasilisha wakiambatanisha na samasi ama forodha ya kesi. Alidai kuwa upande wa utetezi wana Mawakili zaidi ya wawili na kwamba kutokana na mazingira hayo Mawakili waliopo wanaweza kuendelea na kesi na akasisitiza PH iwe kesho Mei 16,2018 asubuhi ama mchana. Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hadi Mei 16,2018 saa nane mchana ambapo washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali PH. lnstal GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..