Home » News & Politics » Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi

Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi

Written By Global TV Online on Wednesday, Apr 25, 2018 | 02:40 AM

 
Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi Shingo ya kizazi au cervix ni njia ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba. Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo kupitisha mbegu za kiume kuelekea katika mirija ya uzazi ili kupevusha yai, kupitisha damu ya hedhi na pia ndiyo mlango anaopitia mtoto wakati wa kuzaliwa. Kama zilivyo sehemu zingine za mwili, sehemu hii nayo inaweza kupata maradhi ikiwemo saratani. Saratani ya shingo ya kizazi ni mabadiliko ya chembechembe hai zilizo juu au zinazofanana na shingo ya uzazi ambapo huchukua miaka mingi hadi kujitokeza kwake. Ugonjwa huu huchukua zaidi ya miaka 15 mpaka 20 kugundulika lakini kabla ya kujitokeza bayana hutokea mabadiliko kadhaa yanayoweza kugundulika mapema na kufanikiwa kuzuilika katika hatua za mwanzoni. Ugonjwa huu huwaathiri wanawake wengi wa rika zote walio katika umri wa kuzaa. Miaka ya nyuma kabla ya maambukizi ya Ukimwi kansa ya shingo ya kizazi ilikuwa ikiwapata zaidi wanawake wenye umri wa miaka 45 na kuendelea. Instal GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS:http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit MASOGANGE https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..