Home » News & Politics » PROF LIPUMBA: "Maalim Seif Anaibomoa CUF, Anawakumbatia Chadema"

PROF LIPUMBA: "Maalim Seif Anaibomoa CUF, Anawakumbatia Chadema"

Written By Global TV Online on Thursday, Mar 22, 2018 | 05:43 AM

 
PROF LIPUMBA: "Maamlim Seif Anaibomoa CUF, Anawakumbatia Chadema" Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amezungumza na waandishi wa habari leo Machi 22, 2018. Profesa Lipumba amezungumzia kuhusu Mgogoro wa ndani ya chama hicho anaodai kuwa umeanzishwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif, kwa lengo la kukidhoofisha chama na kuwakumbatia viongozi wa Chadema. Profesa Lipumba pia amesema kuwa baraza kuu la Cuf limetambua kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Hamad, amekidhoofisha chama chao kwa kutotekelea azimio la baraza kuu la kufungua kesi Mahakama kuu ya Zanzibari, kupinga kufutwa matokeo ya Uchaguzi wa wawakilishi na madiwani ambao walikabidhiwa hati za ushindi kwenye majimbo yao, baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, 2015, ambapo kesi hizo zingefunguliwa Cuf ingekuwa na wawakilishi 27 wa Majimbo na nusu ya wawakilishi wote wa viti maalum. Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..