Home » News & Politics » “Mimi sitoi maelekezo, natoa muda mfanye wenyewe” –Dr Tulia

“Mimi sitoi maelekezo, natoa muda mfanye wenyewe” –Dr Tulia

Written By Millard Ayo on Tuesday, Nov 21, 2017 | 08:24 AM

 
Naibu Spika Dr Tulia Ackson alikuwa Tanga baada ya kualikwa na Mbunge wa jimbo la Mlalo Rashid Shangazi kwa ajili ya uzinduzi wa ujenzi wa wodi ya wazazi katika kituo cha afya Mlalo wodi iliyopewa jina la Dr Tulia lengo likiwa ni kupunguza vifo vya kinamama na watoto ambapo Dr Tulia ameahidi kuchangia shilingi Milion 5 pamoja na mifuko 300 ya cement ili kusaidia ujenzi huo kumalizika haraka. Dr Tulia pia alienda hadi katika tarafa ya Mtae ambapo huko alikutana na vikundi vya kuweka na kukopeshana (VICOBA) ambapo walimwelezea changamoto mbalimbali zinzzowakabili huku akishangazwa na baadhi ya viongozi kushindwa kuzitatua.