Home » People & Blogs » Young Dee Awasemea Mbovu Dogo Janja na Young Killer, Awaita Vifaranga

Young Dee Awasemea Mbovu Dogo Janja na Young Killer, Awaita Vifaranga

Written By Global TV Online on Friday, Sep 22, 2017 | 09:08 AM

 
Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 MSANII wa HipHop nchini, Young Dee, anayetamba na ngoma yake mpya ya Utani Utani ametoa povu juu ya kauli ya Young Killer, pale Young Killer aliposema kuwa Young D na Dogo Janja hata wakiingia studio wote halafu wafanye ngoma ya pamoja, na yeye Young Killer aingie studio afanye ngoma yake peke yake, bado hawatamfikia hata wafanyeje. Pia Young Killer alisema kuwa mashabiki wasimfananishe na hao watu kwani haendani nao hata kidogo. Alichofunguka Young Dee kuhusu kauli ya Young Killer kusema hawamuwezi, ni kuwa Young Killer na Dogo Janja ni vifaranga vyake, kwa hiyo hawamuwezi hata kidogo. Alipoulizwa kama ikitokea shoo ya pamoja baina ya yeye, Dogo Janja na Young Killer, alisema uwezo wake ni mkubwa sana, hawezi kufanya shoo kwenye jukwaa moja nao. ”Inategemea hiyo shoo imeandaliwa kwa aina gani kwa sababu mimi sasa hivi nimekua, kwa hiyo siwezi kufanya shoo ya pamoja na hao vifaranga vyangu. Sidhani kama itakuwa shoo nzuri kwa mashabiki zangu kwa sababu mimi nikiwa jukwani ni mtu mkubwa sana. Ukiwakusanya wote hao labda ndiyo unaweza kupata nusu ya Young Dee,” alisema Young Dee Siku zote hamna msanii ambaye anakubali kufunikwa lakini hii ya hawa vijana wanaofanya muziki wa HipHop imekuwa balaa pale kila mtu anapojiona yupo juu ya mwenziye, lakini wote ni wakali wa HipHop kutoka Tanzania kwenye kisiwa cha burudani. FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli... https://www.youtube.com/watch?v=XEYQREHqBrU