Home » People & Blogs » Rais Magufuli na Rais Museveni kuweka jiwe la msingi mradi wa bomba la mafuta Hoima Tanga

Rais Magufuli na Rais Museveni kuweka jiwe la msingi mradi wa bomba la mafuta Hoima Tanga

Written By press statehouse on Friday, Jul 28, 2017 | 09:36 AM

 
Tarehe 05 Agosti, 2017 siku ya Jumamosi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wataweka jiwe la msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Mradi huu ni moja ya miradi mikubwa ambayo nchi yetu imeipata na kuanza kutekeleza tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani tarehe 05 Novemba, 2015. Ni mradi ambao uwekezaji wake ni mkubwa wa Dola za Marekani Bilioni 3.5 sawa na takribani Shilingi Trilioni 8 za kitanzania.