Rais John Magufuli amefungua kiwanda cha vifungashio cha Global Packaging (T) LTD mjini Kibaha asubuhi ya Juni 21, 2017 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu ya mkoa wa Pwani.
Akiwa kiwandani hapo, mheshimiwa rais alioneshwa jinsi uzalishwaji wa bidhaa mbalimbali, ikiwemo mifuko ya sandarusi inavyotengenezwa mpaka kukamilika.
Mheshimiwa Rais yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Pwani ambapo amewahutubia wakazi wa Kibaha katika Uwanja wa Bwawani. Katika hotuba yake ya Kibaha, mheshimiwa rais amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Pwani kwamba neema inakuja siku chache zijazo kwa sababu lengo lake ni kuwakomboa wananchi kiuchumi, akaongeza kwamba ujenzi wa reli ya standard gauge na bandari kavu ya Ruvu, vitakuwa na faida kubwa kwa wakazi wa Pwani.
Mheshimiwa rais ameendelea kueleza kwamba kwa kutumia miradi hiyo mikubwa miwili, anaamini wananchi wa mkoa wa Pwani hasa maeneo ya Kibaha na Ruvu, watanufaika sana kibiashara.
Mheshimiwa rais aliongeza pia kwamba kuna ujenzi mwingine wa barabara kubwa yenye njia sita kutoka Dar es Salaam mpaka Chalinze, ikiwa na fly-overs zaidi ya saba ambayo itakuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Pwani na Tanzania kwa jumla.
Rais Magufuli yupo mkoani Pwani kwa ziara ya kikazi kwa siku tatu.
Akizungumza na wananchi wa Kibiti na Rufiji, mheshimiwa rais ametoa tamko zito kwa wakazi wa Kibiti na Rufiji na kueleza kwamba watachelewa kupata maendeleo, ikiwemo kujengwa kwa viwanda, kwa sababu ya vitendo vya uhalifu wanavyoviendekeza.
Mheshimiwa Magufuli amesema wananchi wa Rufiji na Kibiti wanawajua wahalifu lakini wanawaficha na kukataa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo.
Amewatahadharisha wote wanaoendeleza vitendo vya kihalifu Kibiti na Rufiji kwamba serikali yake siyo ya kuchezewa, atahakikisha anawanyoosha. Akawataka kama wanamsikia, wapeleke salamu kwa wenzao kwamba serikali yake siyo ya mchezo.
Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
http://www.youtube.com/c/uwazi1
http://www.youtube.com/c/uwazi1
http://www.youtube.com/c/uwazi1
WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/
FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublishers/
TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari
INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpublishers/