Home » People & Blogs » Msukama - Ni Bora Kuishia la Saba Kuliko Kuwa na Vyeti Halafu Huna Akili

Msukama - Ni Bora Kuishia la Saba Kuliko Kuwa na Vyeti Halafu Huna Akili

Written By Global TV Online on Friday, Jun 30, 2017 | 02:33 AM

 
Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Bunge limebadili ratiba kwa Bunge kuendelea na shughuli zake hadi Julai 5 mwaka huu, ambapo bunge hilo litaahirishwa. Alisema Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2017 kwa kuangalia upungufu uliojitokeza itafanyiwa kazi na Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohammed Mchengerwa. Ndugai alisema pia Bunge limeunda kamati maalumu itakayoundwa na wajumbe wa kamati nne za Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Kamati ya sheria Ndogondogo na Kamati ya Katiba na Sheria, itakayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dotto Biseko ambayo itapitia miswada miwili ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka 2017. Pia kamati hiyo itafanyia kazi Muswada wa Sheria ya Mamalaka ya nchi kuhusu Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017. Akizungumza bungeni jana Mbunge wa Geita, Jopseph Kasheku Msukuma aliwaponda upinzani ambao hawakutaka mswada huo uanze kujadiliwa na badala yake wapewe muda wa kuusoma na kutafakari zaidi kabla ya kuanza kuchangia na kuupitisha kuwa sheria. kwa upande wake, Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara alimcharukia Msukuma na kumwambia kuwa hana haja ya kuelewa mambo mengi kwenye huo mswada kwani alishajipambanua kwamba yeye ni darasa la saba. Jambo hilo lilipelekea Msukuma kumjibu kuwa Ni Bora Kuishia la Saba Kuliko Kuwa na Vyeti Halafu Huna Akili WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublishers/ TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpublishers/