Home » News & Politics » Kamanda Sirro: Askari Aliyemfyatulia Risasi Adam Malima Alikuwa Anajilinda

Kamanda Sirro: Askari Aliyemfyatulia Risasi Adam Malima Alikuwa Anajilinda

Written By Global TV Online on Tuesday, May 16, 2017 | 11:06 AM

 
Kamanda Sirro aongea kuhusu Askari aliyefyatua risasi mbele ya Waziri wa zamani Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, leo amezungumza na waandishi wa habari akieleza juu ya mzozo uliotokea baina ya aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya awamu ya nne, Adam Malima na Polisi katika eneo la Masaki lililopelekea askari huyo kufyatua risasi kadhaa hewani. Kamishna Sirro alieleza kuwa Mheshimiwa Adam Malima alikuwa ameegesha gari lake eneo ambalo haliruhusiwi kwa ajili ya maegesho ndipo alipokuja mfanyakazi wa kampuni ambayo ni wakala wa ukusanyaji wa madeni, kukamata teksi bubu pamoja na magari yaliyoegeshwa vibaya akiamuru gari la Malima lipelekwe “yard” ya kampuni hiyo. Lakini dereva wa Malima likataa na akaamua kuondoa gari katika eneo lilipokuwa limeegeshwa, ndipo askari wa Polisi alipoingilia tukio lile. WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublishers/ TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpublishers/ Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chaneli yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1