Home » News & Politics » Wasanii Bongo Movies Wampinga Wema Sepetu, Wakanusha Kuidai CCM

Wasanii Bongo Movies Wampinga Wema Sepetu, Wakanusha Kuidai CCM

Written By Global TV Online on Tuesday, Feb 28, 2017 | 04:57 AM

 
Wasanii wa Bongo Movies waliokuwa wakishiriki kwenye kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ya Mama Ongea na Mwanao, wamezungumza na waandishi wa habari na kutoa msimamo wao kuhusu madai yaliyotolewa na mwanadada Wema Sepetu, kwamba wanakidai Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku aliyekuwa mwenyekiti wa kampeni kwa upande wa wasanii, Steve Nyerere akisema hakuna anayedai chochote. Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea, wasanii has wakiongozwa na Yobnesh Yusuph 'Batuli' na Ndumbangwe Misayo 'Thea', wamesema madam aliyoyatoa Wema Sepetu hayana ukweli wowote kwa sababu wasanii wote walilipwa na Wema alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakiwalipa wasanii wengine. Mara bade ya kuzungumza manna machache, mkutano huo na waandishi wa habari ulimalizika, ukiwa umechukua dakika chache tu. BONGO MOVIES| WASANII| WEMA SEPETU| STEVE NYERERE|BATULI|KAMPENI YA CCM| MAMA ONGEA NA MWANAO|