Home » News & Politics » Kijiji cha Wachawi

Kijiji cha Wachawi

Written By Citizen TV Kenya on Saturday, Sep 14, 2013 | 12:57 AM

 
Zaidi ya familia 13 katika kijiji cha Nyandeho kaunti ya Siaya wamelazimika kulala nje kufuatia visa vya moto wa ajabu unaoendelea kuchoma nyumba zao kwa muda wa wiki moja sasa. Wanakijiji hao wamepoteza mali katika visa hivyo vya moto wakisema kuwa ni nguvu za uchawi zinazosababisha moto huo. Na kama anavyotueleza Pheona Kengah sasa inawabidi wanakijiji hao kutafuta suluhu mbadala ambalo ni maombi ili kukabiliana na hali hiyo.