Home » News & Politics » Uhuru na Raila wakutana

Uhuru na Raila wakutana

Written By KTN News Kenya on Saturday, Apr 13, 2013 | 03:03 PM

 
Rais Uhuru Kenyatta na naibu william Ruto leo walikutana na kufanya mazungumzo na waliokuwa wapinzani wao wakuu, katika uchaguzi mkuu uliopita, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka. Mkutano wa leo ikulu unafuatia msururu wa mazungumzo kupitia njia ya simu kati ya rais Kenyatta, na Odinga aliyekuwa waziri mkuu. Katika mkutano wa leo rais Uhuru Kenyatta alikubali kuupiga jeki ulinzi wa raila na kalonzo na sasa watapewa walinzi 12 kila mmoja.kulingana na duru za ikulu, rais Kenyatta ndie amekuwa mstari wa mbele kusisitiza kuwepo kwa mkutano huu, na Raila Odinga hakukataa kunyooshewa mkono na aliyekuwa mpinzani wake mkuu. Mkutano wa leo pia ulikubaliana cord wasimamie kamati mbili muhimu za bunge. Ali Manzu anatufungulia jamvi la ktn leo wikendi Watch KTN Streaming LIVE from Kenya 24/7 on http://www.ktnkenya.tv Follow us on http://www.twitter.com/ktnkenya Like us on http://www.facebook.com/ktnkenya